February 3, 2015


Kikosi cha Yanga, kimetua salama mjini Tanga kujiandaa na mchezo wake wa kesho dhidi ya Coastal Union.


Lakini Yanga wamekataa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambao walitakiwa kufanya mazoezi leo na kuamua kufanya mazoezi kwenye uwanja wa jeshi.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema walipanga kufanya mazoezi kwenye uwanja huo na si Mkwakwani.
“Nafikiri hakuna tatizo, kilichotakiwa pale ni suala la mazoezi na tumefanya, hivyo hakuna tatizo lolote,” alisema Muro.


Yanga ina kibarua cha kuivaa Coastal Union kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic