Kipa wa Simba, Ivo Mapunda ambaye alisababisha hofu kwa wadau wa
timu yake kutokana na kuchanika juu ya jicho katika mechi ya Ligi Kuu Bara
dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri wiki iliyopita, amepata nafuu na
ameanza mazoezi pamoja na wenzake jana Alhamisi.
Mara baada ya kuumia, Ivo alitolewa uwanjani katika mchezo huo na
kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi kisha nafasi yake kuchukuliwa na Peter
Manyika.
Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, alisema hali ya kipa huyo kwa
sasa ni nzuri na alianza mazoezi tangu jana Alhamisi baada ya maendeleo yake
kuwa mazuri kwa kiasi kikubwa.
Gembe aliongeza kuwa, kwa upande wa beki wa timu huyo ambaye naye
alipata majeraha ya mgongo katika mchezo huohuo wa Polisi, Hassan Kessy
anaendelea vizuri.
“Kessy pia ameanza mazoezi kama kawaida baada ya kupata matatizo
kidogo katika mchezo uliopita lakini sasa yupo fiti na wachezaji wengine kwa
jumla wanaendelea vizuri,” alisema Gembe.
Simba inatarajiwa kukipiga dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa
Kambarage ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Bara.







0 COMMENTS:
Post a Comment