![]() |
| MGOSI... |
Baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya BDF XI,
kupitia kwa straika mahiri wa kikosi cha Yanga, Amissi Tambwe, straika wa
Mtibwa, Musa Hassan Mgosi ameibuka na kusema kuwa Tambwe ni hatari na ni mmoja
wa wachezaji ambao kwake anaona wanastahili kuitwa bora nchini Tanzania.
Tambwe alifanikiwa kuzifumania nyavu mara mbili dhidi ya BDF XI,
katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar.
Mgosi amesema kuwa siku zote amekuwa akimkubali Tambwe kutokana
na uwezo wake wa hali ya juu, hivyo alikuwa akimsubiri kwa hamu aifurahishe
nafsi yake kama vile ambavyo alifanya wikiendi iliyopita.
“Ninapoitaja orodha yangu ya wachezaji bora Tanzania, Tambwe hawezi
kukosa kwa sababu ni mchezaji ambaye ninamkubali sana, kikubwa amenifurahisha
zaidi alipoifunga BDF XI.
“Ninawapongeza wachezaji wa Yanga kutokana na umoja wao
waliouonyesha kwenye mchezo mbele ya wageni kutoka Botswana, nawaomba wasishibe
sifa na wakafanye kweli kwenye mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo,” alisema
Mgosi.








0 COMMENTS:
Post a Comment