| KIFARU (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA MMILIKI WA BLOGU YA SALEHJEMBE, SALEH ALLY. |
Hayo ni maneno ya msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru ambaye ameiambia SALEHJEMBE kuwa mateso ya Mtibwa Sugar ni ya muda.
"Kweli tumekuwa hatuna mwendo mzuri hasa baada ya kutoka katika michuano ya Mapinduzi kule Zanzibar.
"Mtu anayeweza kubadilika ni yule anayekubali alipojikwaa, anakubali watu amekosea. Sasa tunajua wapi tulikosea na tunaendelea kurekebisha makosa.
"Ukirekebisha makosa, basi una uhakika wa kurudi katika ubora wako na Mtibwa Sugar itarudi na wengine watashangaa sana," alisema Kifaru.
Mtibwa Sugar imekuwa ikipoteza mechi mfululizo au kuambulia sare hali inayoshangaza kwa timu hiyo iliyokuwa hajapoteza mechi kwa kipindi kirefu kuliko timu yoyotr ya Ligi Kuu Bara katika msimu huu.







0 COMMENTS:
Post a Comment