Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema
anaamini mchezo wa Ligi Kuu Bara kati yao dhidi ya Prisons mjini Mbeya utakuwa
mgumu.
Pluijm ameungana na Kocha Mkuu wa Prisons,
David Mwamwaja aliyesema kikosi chake ni kigumu na imara sana.
Lakini Pluijm raia wa Uholanzi amesema Yanga
imeimarika katika kipindi hiki, hivyo Prisons wawe makini zaidi hata kama wako
kwao.
“Wako ligi kuu, lazima tukiheshimu kikosi
chao. Lakini kwa sasa kikosi chetu tayari kimekaa vizuri.
“Ninaamini wachezaji watakuwa katika ari ya
juu, watacheza kwa umakini mkubwa. Sasa Prisons wasichukulie mambo kwa ulahisi,”
alisema.
Yanga tayari imetua mjini Mbeya na Pluijm
amesisitiza ana matumaini watafanya vizuri katika mechi hiyo ya Alhamisi kabla
ya kuendelea kubaki na kuisubiri Mbeya City.







0 COMMENTS:
Post a Comment