Kocha maarufu nchini Rwanda, Jean Marie
Ntagwabila amefariki dunia.
Ntagwabila alizidiwa kete kidogo na Goran
Kopunovic ambaye ndiye kocha mkuu wa sasa wa Simba.
Wawili hao ndiyo waliingia fainali katika
kuwania kuinoa Simba kuchukua nafasi ya Mzambia, Patrick Phiri.
Habari kutoka Rwanda zimeeleza, kocha huyo
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa
mapafu.
“Kweli kocha hatuko naye tena, amefariki
dunia kwenye Hospitali ya Kanombe inayomilikiwa na jeshi,” alisema mmoja wa
wanahabari wakongwe wa Rwanda, Clever Kazungu.
Ntagwabila aliyewahi kung’ara na APR akiwa
mchezaji na baadaye kocha, pia alizifundisha kwa mafanikio makubwa Atraco,
Rayon na Kiyovu.
SALEHJEMBE: KAZI YA MUNGU KWELI HAINA MAKOSA, KAPUMZIKE KWA AMANI RAFIKI JEAN MARIE
0 COMMENTS:
Post a Comment