Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema hali ya kikosi chake kushindwa kutumia nafasi inachanganya, lakini hawataka tamaa.
Pluijm amekuwa akilia na nafasi nyingi wanazopoteza katika kila mechi.
"Kweli bado ni tatizo, si dogo kwa kuwa kila mmoja anaweza akaliona sasa. Tunahitaji kuendelea kulifanyia kazi, tunahitaji kutulia na hatuwezi kukata tamaa.
"Ukisema tukubali kuchanganyikiwa, tunaweza kujichanganya zaidi. Lakini ni lazima tukubali kuna tatizo na lazima tulitatue," alisema Pluijm.
Wachezaji wa Yanga wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi katika kila mechi, hivyo kuifanya timu yao itoke bila mabao.
Mara ya mwisho, Yanga imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ndanda FC huku washambuliaji wake wakipoteza nafasi takribani saba za wazi za kufunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment