February 3, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic ameonyesha wazi masikitiko yake kutokana na kifo cha ghafla ya Kocha Jean Marie Ntagwabila.

Kopunovic amesema amesikitishwa na taarifa hizo kwa kuwa kocha huyo raia wa Rwanda alikuwa kati ya rafiki na wapinzani wake kikazi.

“Wiki iliyopita nilikuwa nafuatilia habari zake mtandaoni, kwa kweli imenisikitisha sana.

“Wakati nikiwa Polisi Rwanda, alikuwa mpinzani wangu mkubwa akiwa na Kiyovu. Aliwahi pia kufundisha timu nyingine za Rwanda kwa mafanikio makubwa,” alisema raia huyo wa Serbia.

Ntagwabila amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kukimbizwa kwenye hospitali ya kijeshi ya Kanombe jijini Kigali kutokana na matatizo ya mapafu yaliyosababisha ashindwe kupumua.

Simba iliamua kumchukua Kopunovic baada ya kuona wanamhitaji zaidi ya Ntagwabila ambaye pia alikuwa na nafasi ya kuchukua mikoba ya Patrick Phiri raia wa Zambia aliyetimuliwa Simba.

Marehemu aliwahi kuwa mchezaji wa APR na baadaye kocha, pia alizifundisha Rayon na Atraco na kuzipa makombe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic