February 3, 2015


Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemwambia kiungo mkongwe wa Simba, Shabani Kisiga asidhani anausumbua uongozi wa klabu hiyo kwa kuondoka kambini.


Kisiga ameondoka kambini Simba kwa madai amekuwa hachezeshwi, lakini Hans Poppe amesema anajipotezea muda wake.

“Hawezi kutusumbua sisi, aliwahi kutusumbua lakini alirudi na kusema kwamba sasa yuko vizuri.

“Kisiga alisema amekuwa tofauti, lakini sasa ameamua kuondoka jambo ambalo halitusumbui na ingekuwa vizuri afanye utaratibu aende tu kwa amani kuliko kufanya hivyo,” alisema.

Hans Poppe alisisitiza suala la nidhamu huku akisema Kisiga alipaswa kuwa mfano katika suala la nidhamu.
Pia alisema mwenye uwezo wa kuona nani anapaswa acheze ni kocha na kama Kisiga angekuwa anafaa, kamwe Goran Kopunovic asingemuacha nje.


Pia alisema mwenye uwezo wa kuona nani anapaswa acheze ni kocha na kama Kisiga angekuwa anafaa, kamwe Goran Kopunovic asingemuacha nje.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic