Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani leo pale Mkwakwani mkoani Tanga, kukipiga dhidi ya
Coastal Union, lakini upande wa pili ni kuwa makocha wa Simba, Goran Kopunovic
na msaidizi wake, Selamani Matola wanatarajiwa kuwa uwanjani hapo kuishuhudia
mechi hiyo.
Yanga
itakuwa mgeni wa Coastal, katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ikiwa inajiandaa
kukipiga dhidi ya BDF ya Botswana, katika Kombe la Shirikisho, lakini Kopunovic
atakuwa uwanjani hapo akishuhudia mechi hiyo na kuchukua mambo fulani kuhusu
mpinzani wake Hans van Der Pluijm, ambaye ni kocha wa Yanga.
Imefahamika
kuwa Kopunovic na Matola wanatarajiwa kuondoka mapema leo jijini Dar, ili
kuiwahi mechi hiyo wakati timu yao ikitarajiwa kuondoka baadaye mchana kwenda
Tanga ambapo pia itakuwa na mechi Jumamosi ijayo dhidi ya Coastal kwenye uwanja
huohuo wa Mkwakwani.
Mtoa
taarifa kutoka Simba ameliambia gazeti hili kuwa, makocha wao wanaenda kuzisoma
timu zote mbili, Yanga ambao tayari wapo Tanga na Coastal kwa kuwa wanajua wote
ni wapinzani wao kwenye ligi.
“Makocha
wataondoka mapema kesho (leo) nia ni kuiwahi hiyo mechi, unajua Kopunovic bado
ni mgeni wa ligi ya Bongo, ndiyo maana anahitaji kuzijua timu zote kwa ukaribu,”
alisema mtoa taarifa.
Kuhusiana na safari hiyo, Matola alisema kwa ufupi: “Kweli
tutaenda Tanga, ila tuwasiliane baadaye nipo kwenye kikao.”
0 COMMENTS:
Post a Comment