Beki wa Yanga, Mbuyu Twite, raia wa Congo,
ameomba kufungwa kitanzi mapema na timu yake hiyo kwa kusema kuwa yupo tayari
kuongeza mkataba iwapo uongozi wa timu hiyo utafanya hivyo.
Twite aliyesajiliwa Yanga msimu mmoja
uliopita, anatarajia kumaliza mkataba wake na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu
mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Twite
alifunguka kuwa yupo tayari kuongeza mkataba Yanga iwapo watamhitaji na kudai
kuwa kuna timu ambazo zinamfuatilia kwa sasa lakini hawezi kuziweka wazi.
“Mkataba wangu na Yanga unatarajiwa kumalizika
mwishoni mwa msimu huu mara baada ya kumalizika kwa ligi, hivyo nipo tayari
kuongeza mkataba mwingine iwapo viongozi watahitaji.
“Yanga ni timu ninayoipenda sana hapa Tanzania
lakini siwezi kusema ni timu gani ambazo zinanifuatilia kwa sasa, hiyo ni siri
yangu hata kama zipo,” alisema Twite ambaye amekuwa na uwezo mkubwa wa kurusha
mipira.
0 COMMENTS:
Post a Comment