Yanga
imerejea kileleni Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0.
Ushindi huo
umeifanya Yanga kufikisha pointi 48 dhidi ya Azam FC yenye 46 ambayo
imelazimishwa sare ya bila mabao dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Yanga imebuka
na ushindi huo mnono kwenye Uwanja wa ugenini wa Sokoine jijini Mbeya ikiwa ni
baada ya viungo wake Simon Msuva na Andrey Coutinho kufunga.
Msuva
amepachika mabao mawili, huku Coutinho na kukamilisha idadi ya tatu bila dhidi
ya kikosi cha David Mwamwaja ambaye alitamba leo ingekuwa kazi ngumu kwa Yanga.
Pamoja na
kuwa ugenini, Yanga walitawala mchezo kwa vipindi vyote huku wakipoteza nafasi
nyingi za kufunga.
Mara kadhaa,
Prisons nao walijitutumua hata hivyo kwa dakika zote 90 walifanikiwa kufanya
mashambulizi makali au makubwa matatu tu.
Kwa kipigo
hicho, Prisons inaendelea kubaki mkiani ikiwa na pointi 11 hivyo kuwa katika
wakati mgumu na hofu ya kuteremka daraja.










Jamani yanga noma
ReplyDelete