Kocha Mkuu wa BDF XI, Letang Kgengwentang amesema hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam itakuwa changamoto kwao wakati wanaivaa Yanga leo katika Uwanja wa Taifa kwa kuwa inatofautiana sana na kwao katika jiji la Gaborone nchini Botswana.
BDF ni wageni wa Yanga leo katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
“Hali ya hewa ya hapa (Dar) ni tofauti na ya nyumbani, hiyo ni
changamoto kubwa kwetu. Huku kuna joto sana.
“Nilipokuwa mchezaji niliwahi kukutana na wachezaji wa Tanzania,
nawajua staili yao ya uchezaji, nia yetu ni kushinda, tena ushindi wa mabao
mawili.
“Yanga ya sasa ni tofauti na ile ya msimu uliopita, inacheza sana
soka la kuzuia ndiyo maana wanafunga mabao machache lakini ile iliyopita
ilikuwa inacheza soka la kushambulia na hata katika mechi zao walikuwa wakifunga
mabao mengi.”







0 COMMENTS:
Post a Comment