February 21, 2015


Katika kile kinachoonekana kuwa na imani za kishirikina, watu wanaodhaniwa kuwa ni Mbeya City juzi mara baada ya mchezo kati ya Yanga na Prisons kumalizika, waliingia kwenye Uwanja wa Sokoine uliopo mjini hapa kwa ajili ya kufanya lindo ili ‘usiharibiwe’.


Watu hao walionekana kutokuwa na imani na kila mtu aliyekuwa akikatiza katika nyasi za uwanja huo, ambapo walionyesha ukali kwa kila aliyekiuka na hali kama hiyo ilimkuta pia shabiki maarufu wa Yanga anayetumia staili ya kujipaka masizi usoni na kujaza nguo nyingi tumboni, maarufu kama Ally Yanga.


Shuhuda wetu, alishuhudia watu hao mara baada ya mahojiano ya makocha wa Prisons na Yanga wakikataza kupitia hata kando ya uwanja huo kwa kudai kuwa kuna watu wanataka kufanya uchawi.

“Tupo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa uwanja hauharibiwi kwa chochote, iwe imani za kishirikina au kwa njia nyingine, wenzetu wamefungwa hapa na hatutaki na sisi kupoteza mchezo,” alisema mtu huyo aliyekataa kutaja jina lake.

Katika hatua nyingine, kikosi cha Mbeya City kilikuwa mafichoni tangu Yanga ilipowasili Jumatatu katika jiji hilo na kujifua kulinda heshima ya nyumbani.

Yanga haijawahi kuifunga Mbeya City katika Uwanja wa Sokoine tangu ilipopanda ligi kuu msimu uliopita na kesho wanakutana kwa mara ya pili kwenye uwanja huo.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic