Kocha
wa Chelsea, José Mourinho amesema anapaswa kupewa shukurani kubwa na taifa la
Wafaransa kutokana na kuwapa nafasi wachezaji Frenchmen Raphaël Varane na Kurt Zouma wakiwa na miaka kati ya 20na
21.
"Shirikisho
la Soka la Ufaransa linapaswa kunipa shukurani kubwa kwa kuwa sasa wana mabeki
wawili bora kabisa duniani. Mimi ndiyo nilitoa nafasi kwao ya kuwaamini,”
alisema Mourinho.
Varane
yuko Real Madrid ambako Mourinho alimuacha na alianza kumpa nafasi baada ya
kufarakana na Pepe.
Licha
ya umri wake mdogo wa miaka 20 lakini alimuamini zikiwemo kubwa na akafanya
vema.
Zouma
naye mwenye miaka 21, pia amekuwa akiendelea kupata nafasi katika kikosi cha
Chelsea, hali ambayo imekuwa ikizidi kumuimarisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment