Pamoja na kelele za mashabiki wa Prisons kumtaka kocha wa timu hiyo,
David Mwamwaja kuondoka klabuni hapo kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo,
kocha huyo amefunguka na kusema: “Hatoki mtu hapa.”
Kocha huyo amesema hayo baada ya kusikia minong’ono juu ya ajira
yake hiyo na kusisitiza kuwa anafanya kazi yake kwa ufasaha, lakini wachezaji
ndiyo wanamuangusha kwa sababu wanashindwa kuzitumia nafasi zao na kufuata
maelekezo.
Mwamwaja, alisema kuwa hatishwi na maneno ya watu ambayo kwa upande
wake anaona ni sawa na kumpigia ‘mbuzi gitaa’ kwani hayana msingi wowote zaidi
ya kujenga chuki na uhasama.
“Napenda kuwahakikishia mashabiki wanaodhani naweza kuondolewa
kizembe, wajue kuwa si rahisi kama wanavyofikiri, kwa sababu sioni kosa langu,
nafanya kazi vizuri ila wachezaji ndiyo wanashindwa kutumia nafasi uwanjani.”







0 COMMENTS:
Post a Comment