February 10, 2015

MALINZI AKIWA NA RAIS WA CAF, ISSA HAYATOU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Bw Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) Bw Issa Hayatou kwa kufanikiwa kuandaa salama fainali za Mataifa Afika nchini  Equatorial Guinea bila ya kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.

Katika salamu hizo kwenda kwa Bw Hayatou na nakala yake kupitia Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Bw Hicham El Amrani, Bw Malinzi amesema kwa pamoja analipongeza Shirikisho hilo na wenyeji wa michuano kwa kufanikiwa kuandaa mashindano hayo na kumalizika salama.
IMETOLEWA NA TFF

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic