MSEMAJI WA TFF, BARAKA KIZUGUTO |
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF amepeleka salamu za rambirambi kwa Rais Mohamed Gamal wa Chama cha mpira wa miguu nchnii Misri (EFA ),kufuatia vifo vya mashabiki vilivyotokea mwishoni wa wiki katika mchezo uliowakutanisha Zamalek na ENPPI.
Mashabiki wapatao ishirini na moja (22) wameripotiwa kupoteza maisha katika vurugu hizo zilizowahusisha mashabiki wa Zamalek na ENPPI na kupelekea Shirikisho la Soka nchini Misri kuisimamisha michezo ya Ligi nchini humo.
Katika salam zake, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewaomba wapenzi wa soka nchini Misri kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha maombelezo ya vifo vya mashabiki hao.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA TFF, BARAKA KIZUGUTO
0 COMMENTS:
Post a Comment