Na Saleh Ally
BAADA ya sare ya bao 1-1
juzi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London, sasa Chelsea na Manchester
City hakuna mbabe zaidi ya mwenzake zinapokutana.
Kwani hiyo ni mechi ya pili
ya Ligi Kuu England msimu wa 2014-15 zinakutana na inaonekana hakuna mbabe
zaidi ya mwingine lakini hilo linaweza kupata majibu katika mbio za ubingwa.
Chelsea wapo kileleni
wakiwa na pointi 53 na Man City wanaoigombea nafasi hiyo kwa nguvu zote, wako
katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 48.
Kwa haraka kuna mambo
mawili, kwanza unaweza kuona kama ni mbali sana hadi ubingwa utakapopatikana
kwa kuwa timu zote zimebakiza mechi 15 za mzunguko wa pili.
Pili, kila timu inajua ugumu wake kwa kuwa katika hesabu za
mechi 15 zilizobaki, kuna mabonde ya kila aina kwa kuwa kila timu inapiga
hesabu namna ya ushindi dhidi ya timu kadhaa.
Chelsea na Man City si
kwamba hadi sasa zina uhakika wa asilimia mia kutwaa ubingwa kwa kuwa timu
zilizo katika nafasi ya tatu na nne kama Manchester United, Southampton na hata
Arsenal zinaweza kufanya lolote kwa kuwa soka, mambo yake hayaeleweki.
Lakini ukienda kwa hali
inavyojionyesha kwa sasa, hakuna ubishi timu hizo mbili za majiji ya London na
Manchester ndizo zenye nafasi kubwa ya kuwa na ubingwa, aidha Chelsea wauchukue
au Man City waubakize.
Mechi 15:
Katika mechi 15 zilizobaki kwa
kila timu, ndani yake kuna kila aina ya burudani kutokana na wanakutana na timu
gani.
Timu kubwa tatu za Arsenal, Man United, Southampton,
Liverpool, Tottenham na Everton ndizo zitakuwa kizingiti kikubwa kwa timu hizo.
Karibu kila timu itakutana na
asilimia 90 ya timu hizo na hapo kutakuwa na mtihani mzito kwa kuwa “big match”
mara nyingi inakuwa haina mwenyewe.
Haitabiriki:
Pamoja na presha kwa
makocha Manuel Pellegrini wa Man City na Jose Mourinho wa Man City, inaweza
kuwa katika mechi zinazohusisha timu kubwa kama Arsenal, Liverpool na nyingine,
lakini wanajua ugumu wa Premier League kwani hata timu zinazoonekana ndogo kama
Crystal Palace, West Brom au West Ham zinaweza kutibua mambo na kubadili
uelekeo.
Hivyo watakuwa na presha
kila dakika za kila mechi hadi ligi itakapofikia ukingoni na mwishowe tamati.
Nyumbani & ugenini:
Hii ni presha nyingine kwa
kila timu kati ya hizi mbili. Kila moja inaangalia uchezaji wa nyumbani na
ugenini. Kuna msemo kuwa mpira wa sasa hauna nyumbani wala ugenini.
Lakini ukweli unabaki
palepale kuwa nyumbani ni nyumbani tu, hilo halikwepeki ingawa usipokuwa
makini, inawezekana faida isiwe kubwa pia.
Katika mechi 15, Chelsea ina mechi tisa za nyumbani ambazo ni
nyingi zaidi na sita za ugenini wakati Man City itabaki nyumbani mara nane na
ugenini mechi saba.
Ingawa Chelsea ina mechi
nyingi zaidi za nyumbani, lakini takwimu zinaonyesha kila timu itacheza mara
nyingi nyumbani kabla ya kutoka ugenini.
Je, mechi za nyumbani
zinaweza kuisaidia zaidi Chelsea? Kama watakuwa makini na kuhakikisha
hawapotezi hata pointi moja Stamford Bridge, basi watakuwa na nafasi nzuri ya
kuendelea kubaki kileleni lakini wakiteleza, City ingawa wana mechi pungufu za
nyumbani, wanaweza kufanya vizuri zaidi yao.
Chelsea na Man City hazina mashabiki wengi kama ilivyo kwa
Liverpool na Man United. Lakini ndiyo timu zilizoshikilia soka la England kwa
msimu huu.
Sasa hata kama mambo
yatabadilika, lakini wakongwe hao wanaonekana kazi yao kubwa ni kuwatibulia
kuwa mabingwa au kugombea nafasi nne za juu ili waweze kushiriki Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Vita hiyo ya Chelsea na Man
City si ndogo, inaanzia kwa wamiliki wa timu, mamilionea wa Kiarabu na Kirusi.
Pia makocha maarufu, lakini vikosi vilivyoshiba mamilioni ya pauni. Nani
atashinda mwishoni? Fuatilia kimyakimya.
CHELSEA
Februari 7, 2015
Aston Villa v Chelsea
Februari 11, 2015
Chelsea v Everton
Februari 21, 2015
Chelsea v Burnley
Februari 28, 2015
Leicester City v Chelsea
Machi 1, 2015
Chelsea v Tottenham
Machi 4, 2015
West Ham v Chelsea
Machi 15, 2015
Chelsea v Southampton
Machi 22, 2015
Hull City v Chelsea
Aprili 4, 2015
Chelsea v Stoke City
Aprili 11, 2015
QPR v Chelsea
Aprili 18, 2015
Chelsea v Man United
Aprili 25, 2015
Arsenal v Chelsea
Mei 2, 2015
Chelsea v Crystal Palace
Mei 9, 2015
Chelsea v Liverpool
Mei 16, 2015
West Brom v Chelsea
Mei 24, 2015
Chelsea v Sunderland
MANCHESTER CITY
Februari 7, 2015
Man City v Hull City
Februari 11, 2015
Stoke v Man City
Februari 21, 2015
Man City v Newcastle
Machi 1, 2015
Liverpool v Man City
Machi 4, 2015
Man City v Leicester
Machi 14, 2015
Burnley v Man City
Machi 21, 2015
Man City v West Brom
Aprili 4, 2015
Crystal Palace v Man City
Aprili 11, 2015
Man Utd v Man City
Aprili 18, 2015
Man City v West Ham
Aprili 25, 2015
Man City v Aston Villa
Mei 2, 2015
Tottenham v Man City
Mei 9, 2015
Man City v QPR
Mei 16, 2015
Swansea v Man City
Mei 24, 2015
Man City v Southampton
CHELSEA
MECHI
Nyumbani-9
Ugenini-6
MAN CITY
MECHI
Nyumbani-8
Ugenini-7
0 COMMENTS:
Post a Comment