February 2, 2015


Ivory Coast imeitwanga Algeria kwa mabao 3-1 katika mechi ya Kombe la Mataifa Afrika hatua ya robo fainali.


Mabao mawili ya Bony Wilfred aliyejiunga na Manchester City akitokea Swansea na moja la Gervinho yalitosha kuizima Algeria iliyoonyesha soka safi.

Hata hivyo haikuwa kazi lahisi, kwani pamoja na Tembo hao kuanza kufunga, lakini Algeria walisawazisha na kuwapa wakati mgumu Waafrika hao wa Magharibi.


Uwezo wa wachezaji mmojammoja kwa Ivory Coast pia ulichangia kuongeza uwezo wa kikosi hicho ambacho sasa kitakutana na DR Congo katika mechi ya nusu fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic