Yanga imesema kuwa haina mkanda wala haijaona
mechi yoyote ya wapinzani wao BDF, lakini wanajua kuwa wana wachezaji kutoka Zambia.
Yanga itavaana na BDF XI ya Botswana
keshokutwa Jumamosi lakini inasema itaingia kwa tahadhari zote kwa kuwa wageni
hao ni bora sana.
Kocha
msaidizi wa timu hiyo, Charles Mkwasa, ameliambia Championi Jumatano kuwa,
wamejitahidi kadiri ya uwezo wao kuhakikisha wanapata video za timu hiyo ili
waweze kuwaona lakini imeshindikana.
“Kuhusu wapinzani wetu hao hatuwajui ipasavyo, lakini tunasikia kuwa ni wazuri na wana wachezaji kama watatu hivi kutoka Zambia ambao wanadaiwa kuwa ni wazuri sana na wana akili sana uwanjani.
“Tumejitahidi kutafuta video zao ili tuweze
kuwaona lakini imeshindikana, hivyo tumeamua suala hilo kuliachia uongozi na
sisi tuendelee na kazi yetu ya kuhakikisha tunakuwa vizuri kwa ajili ya mechi
hiyo,” alisema Mkwasa.







0 COMMENTS:
Post a Comment