Baada ya kukaa nje kwa muda wa miezi mitatu kutokana na majeraha ya mguu, kipa namba moja wa Simba, Hussein Shariff ‘Casillas’ amesema amerudi kuitumikia klabu hiyo kwa moyo mmoja.
Casillas tayari ameanza mazoezi tangu Alhamisi ya wiki iliyopita, katika uwanja uliopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Casillas alisema amerudi kuitumikia klabu yake kwa moyo mmoja na kwa kujituma kadiri awezavyo ili kuhahikisha klabu hiyo inafanya vyema msimu huu.
“Mimi nimerudi kuitumikia klabu yangu kwa moyo mmoja, nitahakikisha nafanya vitu tofauti ambavyo vitanitambulisha kama Casillas wa sasa,” alisema Casillas.
0 COMMENTS:
Post a Comment