Timu
ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) inarejea leo mchana saa
8:45, kwa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Misri ambapo jana
ilipoteza mchezo wake wa marudiano kwa kufungwa 9-4 na wenyeji.
Rais
Malinzi amesema timu ya Soka la Ufukweni haikupata matokeo mazuri katika mchezo
wake kutokana na ugeni wa michuano hiyo, uzoefu ndio ulikuwa kikwazo kwa timu
ya Tanzania, kwani ndio mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo ikiwa ni miezi
sita tangu kutambulishwa kwa mchezo huo nchini Tanzania.
Ili
kuwa na timu bora ya Taifa na wachezaji wengi wa mchezo huo, Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini TFF limepanga kuutangaza na kuufundisha mpira wa ufukweni
katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania, tofauti na sasa ambapo mchezo huo
unachezwa Dar es Salaam na Zanzibar.
Katika
mchezo wa jana mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi (3) Kashiru Salum
(1), Tanzania imetolewa kuwania kufuzu kwa fainali za Soka la Ufukweni barani
Afrika na Misri kwa jumla ya mabao 15-6.
Misri
imefanikiwa kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Soka la Ufukweni Visiwa vya
Shelisheli, zitakazofanyika mwezi April mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo
tangu kuanzishwa kwa mchezo huo mwaka 2006 nchini humo.







0 COMMENTS:
Post a Comment