Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma
salama za pongezi kwa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa
kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia 'The
She-polopolo'.
Katika
salam zake Rais Malinzi amesema ushindi walioupata Twiga Stars katika mchezo
huo wa awali, umetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata chini ya kocha mkuu
Rogasian Kaijage, benchi lake la ufundi na TFF.
| MALINZI |
Aidha
Rais amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo wa awali walioupata,
bali wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili
waweze kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa ya Tanzania.
Mchezo
wa marduiano unatarajiwa kufanyika kati ya April 10,11 na 12, 2015, huu jijini
Dar es alaam na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afrika
kwa Soka la Wanawake (All Africa Games Women) zitakazofanyika Brazzavile
Congo Septemba 3-18 mwaka huu.
Twiga
Stars inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku (jumanne) jijini Dar es salaam
kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Zambia.
Kwa
niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF),
watanzania wote wanawapa pongezi Twiga Stars kwa ushindi walioupata wa
awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa marudaiano.
Mabao
ya Twiga Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia (The She-polopolo)
yalifungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).








0 COMMENTS:
Post a Comment