March 12, 2015


 
 Pamoja na kuibuka shujaa kwa klabu yake ya PSG, beki David Luiz raia wa Brazil amewaomba msamaha mashabiki wa Chelsea.



Sare ya bao 2-2 ndiyo iliyoing'oa Chelsea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Luiz akiwa kati ya wafungaji.

Luiz amefunga bao la kwanza la kusawazisha na kuisaidia PSG kuing’oa Chelsea. Awali alitangaza hatashangilia akiwa Stamford Bridge katika mechi hiyo ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa, lakini alishindwa kujizuia baada ya kufunga bao safi la kichwa.

Awali mashabiki walikuwa wakimsomea kila alipokamata mpira na dakika chache baadaye akafunga bao hilo.

Luiz alijiunga na PSG kwa kitita cha pauni milioni 50 akitokea Chelsea.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, beki huyo amewaambia mashabiki wa Chelsea wamuwie radhi kwa kuwa alikuwa akipambana kwa ajili ya kazi yake na hakulenga kuwaumiza miezi yake.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic