Mashabiki
wenye hasira wa Real Madrid wamelivamia gari aina ya Bentley lililokuwa
linaendeshwa na kiungo Gareth Bale na kulipiga mateke na ngumi.
Mashabiki
hao walikuwa na hamu ya kumvaa Bale wakidai hakuisaidia timu hiyo wakati
ikicheza na Barcelona na kupoteza kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja Camp Nou, jana.
Hasira
zao zinatokana na kufungwa lakini ripoti ya magazeti ya leo ya AS na Marca
zimeongeza chuki dhidi ya Bale.
Magazeti
hayo yalionyesha Bale hakuwa na mchango hata punje huku yakikisitiza bei ya
pauni milioni 86 aliyonunuliwa kutoke Tottenham, angalau ingetolewa robo yake
tu wakati wa kumnunua.








0 COMMENTS:
Post a Comment