Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva
amewaomba mashabiki wa Yanga kuendelea kuwaunga mkono.
Akihojiwa mara baada ya mchezo wa leo dhidi ya
JKT Ruvu ambao alifunga mabao mawili, Msuva amesema anaamini wana kazi ngumu na
wataendelea kufanya kama wataungwa mkono.
“Ushirikiano katika timu uko juu na tunataka
kufanya vizuri. Lakini mashabiki watuunge mkono kwa kuwa inatupa nguvu ya
kufanya vizuri zaidi,” alisema Msuva.
Kiungo huyo mwenye kasi wa Yanga amefikisha
mabao 11 na kuongoza katika listi ya wafungaji bora.
Msuva amengoza kwa kumvuka Mrundi Didier
Kavumbagu mwenye mabao 10 ambaye awali ndiye alikuwa kileleni.
0 COMMENTS:
Post a Comment