| SAID FELA (KUSHOTO) AKIWA NA TEMBA NA CHEGGE KATIKA MSIBA WA BONGE LEO. |
Kifo
cha mdau wa muziki na mwanzilishi wa kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge,
kimeendelea kuzua utata baada ya jamaa aliyesababisha kifo chake aliyetajwa kwa
jina la Nasoro kuingia mitini.
![]() |
| MAREHAMU ABDUL BONGE (KUSHOTO) WAKATI WA UHAI WAKE AKIWA NA FELA NA BABU TALE. |
Akizungumza
na mtandao huu mdogo wa marehemu aitwae Idd ambaye aliitwa kuichukua maiti ya
kaka yake muda mfupi baada ya tukio alisema:
"Nikiwa
na marehemu kuna kijana alimuita marehemu akagombelezee ugomvi wa Nasoro na
mkewe na marehemu alipoenda kugombelezea ugomvi huo muda mfupi taarifa zilirudi
kuwa Abdul alianguka na kupoteza fahamu.
“Nilikwenda
kumuangalia nikamkuta ameanguka akiangalia juu huku ameng'ata ulimi,
nilimkimbiza hospitali ya St Monica iliyopo Manzese Darajani ndipo nikaambiwa
kaka yangu amepoteza maisha,” alisema.
Mwili
wa Abdul unatarajiwa kusafirishwea kupelekwa Kijiji cha Mkuyuni kilichopo
Tarafa ya Matombo mkoani Morogoro baada ya taratibu za kipolisi kumalizika.








0 COMMENTS:
Post a Comment