March 23, 2015

DANNY SSERUNKUMA (KUSHOTO) AKIWA JUKWAANI NA WACHEZAJI MAKINDA WA SIMBA, WILLIAM LUCIAN (KATIKATI) NA ABDALLAH SESEME.
Simba ilimsajili mshambuliaji nyota wa Gor Mahia ya Kenya, Danny Sserunkuma. 

Wakati anakuja nchini, Sserunkuma alikuwa ametoka kuichezea timu yake ya taifa ya Uganda kuwania kucheza michuano ya Afcon, lakini wakashindwa katika hatua za mwisho kabisa.

Alikuja nchini baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili, hivyo uzito uliongezeka, kasi ilipungua na ilionekana hakuwa na mazoezi ya kutosha.

Ilionekana alisumbuka sana kuendana na kasi ya Simba na hata Ligi Kuu Bara, lakini alionyesha kuanza kurejea taratibu katika kiwango chake wakati akiwa Kenya ambako alikuwa mfungaji bora msimu uliopita.

Alifanikiwa kuifungia Simba mabao muhimu na kufikisha matatu. Alionekana hakuwa katika kiwango kizuri sana, lakini hakuna ubishi, alitakiwa muda.

Taratibu, Sserunkuma alianza kuwekwa benchi. Yeye mwenyewe alianza kuonyesha mgomo na hata baadaye taarifa za kuwa alisema alikuwa akilazimishwa kufanya mambo ya kishirikina zilizagaa.

Jana ameonekana akiwa jukwaani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar wakati Simba ikipambana na Ruvu Shooting na kushinda kwa mabao 3-0. 

Siwezi kukubaliana na wanaosema Sserunkuma ni garasa. Amekuwa mfungaji bora zaidi ya mara moja, amecheza timu ya taifa ya Uganda yenye wachezaji wengi mahiri lakini amepata nafasi.

Inawezekana anashindwa kuwa bora, huenda ana tatizo, na uongozi au benchi la ufundi linaweza kuzungumza naye kuhusiana na nini asaidiwe.

Lakini kama ameshindwa kabisa, huenda ana bahati mbaya na Simba. Basi aachiwe aende kwa kuwa Simba haiwezi kuwa inaendelea kumlipa zaidi ya dola 1000 (zaidi ya Sh milioni 2.) huku yeye akiendelea kukaa benchi au jukwaani.

Hakuna cha kupoteza, Simba inapaswa ifanye uamuzi mgumu ikiwezekana kumuacha mapema ili isiendelee kuingia hasara.

Simba imekuwa ikihaha kupambana na ukata, sasa si sahihi kuendelea kubaki na mchezaji wa kimataifa anayekaa benchi na kulipwa mshahara bure.

Viongozi wa Simba wanapaswa kuwa wachumi, kusaidia pia kuepusha fedha kupotea bila sababu ya msingi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic