| MANDAWA (KUSHOTO) AKIKABIDHIWA ZAWADI YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI NA WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA. |
Straika nyota wa Kagera Sugar, Rashid Mandawa,
amefunguka kuwa bado hajakata tamaa katika suala la kuwania kiatu cha dhahabu
licha ya kupitwa mabao mawili na straika wa Azam, Didier Kavumbagu.
Mandawa, kwa sasa ana mabao nane, sawa na winga wa Yanga,
Simon Msuvu, huku kinara akiwa Kavumbagu mwenye mabao 10.
Mkali huyo alisema kuwa, furaha yake siku zote ni kuona
kila mchezo anafunga mabao kwa sababu ndiyo kazi yake.
“Msimu huu nitapambana kuhakikisha naibuka mfungaji bora
wa ligi bila kujali nani yupo juu yangu ili kuweza kuwakilisha washambuliaji
wazawa wa hapa nyumbani.”







0 COMMENTS:
Post a Comment