Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, amefungukia
siri ya kung’aa katika kufumania nyavu kwa kusema kuwa, mazoezi binafsi
anayoyafanya ndiyo sababu kubwa.
Msuva ambaye mpaka sasa amecheka na nyavu mara nane
kwenye Ligi Kuu Bara, alisema mara nyingi amekuwa akifanya mazoezi ya kupiga
krosi pamoja na vichwa, hali inayomfanya akiwa uwanjani apate urahisi zaidi wa
kutupia.
“Licha ya kufundishwa na kocha Hans van Der Pluijm,
lakini pia ninakuwa na mazoezi yangu. Naamini hayo yanachangia pia niweze
kufunga nikisaidiana na wenzangu.
“Lakini kuhusu suala la mashabiki kunizomea, binafsi siliangalii
suala hilo, bali ninachokiangalia ni kazi yangu niliyotumwa kufanya na uongozi,
hivyo siwasikilizi hata kidogo kwani ukifanya vizuri ndiyo haohao
wanaokushangilia.”







0 COMMENTS:
Post a Comment