Maisha ya kiungo wa Simba, Shaban Kisiga ndani ya
Msimbazi sasa unaweza kusema ndiyo yamefikia mwisho, kufuatia kauli tata
iliyotolewa jana na uongozi wa klabu hiyo.
Kisiga hajawa na timu tangu Januari 28, mwaka huu baada
ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mbeya City huku kukiwa hakuna mawasiliano
yoyote kati yake na waajiri wake.
Hata hivyo, Katibu wa Simba, Stephene Ally, amekata
mzizi wa fitina baada ya kufunguka kwa kina kuhusu majaaliwa yake kwa kusema
kuwa ni vigumu kurejea Simba kwa kuwa alishindwa kutekeleza masharti.
“Kisiga alijiondoa mwenyewe kikosini, tulifanya kila njia
ya kuwasiliana naye na tukamwambia aandike barua kutueleza sababu iliyomuondoa
kambini bila kuaga lakini amekataa kufanya hivyo.
“Sasa kama anasema anasubiria sisi kumpigia simu,
tutaanzia wapi wakati yeye mwenyewe ameshindwa kutekeleza maagizo? Na tutaanzia
wapi kumtafuta wakati utaratibu unajulikana!
“Cha msingi tunasubiria maamuzi yoyote yatakayofikiwa na
kamati ya utendaji kuhusu suala lake na tutatangaza kama tulivyomtangaza rasmi,”
alisema Ally.







0 COMMENTS:
Post a Comment