Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Genoa, umeisaidia Juventus kuongeza pengo la pointi 14 dhidi ya AS Roma.
AS Roma ndiyo wapinzani wake wao wakubwa na shukurani kwa Carlos Teves ambaye alifunga bao hilo pekee.
Raia huyo wa Argentina ambaye alibeba ubingwa wa England akiwa na Man United na baadaye Man City amezidi kuonyesha umuhimu wake katika kikosi hicho cha Italia.
Wiki iliyopita, Tevez aliisaidia Juve kufuzu katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Dortmund wakati waliposhinda 3-0, ugenini.









0 COMMENTS:
Post a Comment