Mshambuliaji wa Emmanuel Emenike wa Fenerbahce amekuta
akishindwa kujizuia na kulazimisha afanyiwe mabadiliko na kutolewa nje hata
kabla ya kipindi cha pili.
Katika mechi hiyo ya Ligi kuu ya Uturuki dhidi ya wapinzani
wao Besiktas, Emenike raia wa Nigeria alilazimisha kutoka na kuvua jezi wakati
mashabiki walipoanza kumshambulia kwa maneno makali yakiwemo ya kibaguzi.
Mashabiki hao walikuwa wakimzoea baada ya kushindwa kutuliza
mpira mrefu aliopigiwa.
Hali hiyo ilionyesha kumuudhi ingawa mashabiki hao pia
walilalama kwamba msimu huu amekuwa hana msaada kwa timu yao.
Pamoja na kufanikiwa kutoka, Emenike alirudishwa na benchi la
ufundi akiwemo kocha wa timu hiyo ambaye hata hivyo baadaye alilazimika kumtoa
baada ya kipindi cha kwanza kwisha.
Ubaguzi wa rangi umekuwa ukiendelea katika nchi mbalimbali
ikiwemo Uturuki ambayo ndiyo nchini pekee duniani iliyo katika mabara mawili ya
Asia na Ulaya.
Asilimia kubwa ya Waturuki ni wale wenye asili ya Waarabu,
lakini ajabu nao wamekuwa na tabia hizo mbovu za kishenzi za ubaguzi wa rangi.












0 COMMENTS:
Post a Comment