Yanga wameendelea kulikomalia suala la mshambuliaji wa Simba,
Ibrahim Ajibu kucheza kwenye mchezo wa Prisons akiwa na kadi tatu za njano na kusema lazima Simba wakatwe
pointi tatu.
Sokomoko hilo limekuja baada ya TFF kuipa mamlaka Simba kumtumia
Ajibu katika mechi na Prisons iliyopigwa wiki iliyopita huku pia ikimruhusu
kucheza katika mchezo na Yanga hapo kesho wakati alitakiwa kutumikia adhabu
kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, lakini TFF kupitia kwa katibu na
watendaji mbalimbali wamekuwa wakisisitiza kuwa kanuni zao zimefanyiwa marekebisho
tangu Februari, mwaka huu.
Hata hivyo, Yanga pamoja na klabu za Azam, JKT Ruvu, Ruvu
Shooting, Kagera Sugar na Coastal Union zimepinga kuwepo kwa mabadiliko hayo
kwani hakuna taarifa rasmi iliyotumwa kwa klabu husika, zaidi ya Simba tu.
Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amefunguka kuwa katiba barua
hiyo kwenda TFF, wameambatanisha masharti matano na mojawapo likiitaka TFF,
Simba kukatwa pointi sita na kupigwa adhabu kali kama fundisho.
“Hakuna taarifa zozote kuhusu kanuni kubadilishwa, iweje zianze
kutumika ilhali hazijawafikia walengwa? Soka letu limekuwa likiendeshwa
kienyeji zaidi lakini katika hili lazima tusimame kidete kutetea haki yetu.
“Bado tunajiuliza hayo mabadiliko yalifanywa lini na kwa sababu
ipi ya msingi? Tumeamua kuwaandikia barua TFF na ninaipeleka leo (jana) na tunawapa
maazimio yenye masharti matano kuhusu msimamo wetu.
Mojawapo ni watendaji wa Bodi
ya Ligi kujiengua kwa kushindwa utendaji, pili, Klabu ya Simba ipokwe pointi
sita, maana kabla ya Ajibu walikuwa wamemtumia Banda (Abdi) kwenye mchezo na
Coastal kimakosa, maana hakuna aliyejua kama kulikuwa kuna marekebisho ya
kikanuni,” alisema Dk Tiboroha na kufunguka msimamo wao kwa Ajibu kucheza
mchezo wa kesho.
“Sisi hatuna shida na mchezaji, wao wakitaka wamtumie maana
watakuwa wanaturundikia pointi. Acheze tu, tutajua mbele kwa mbele.”
0 COMMENTS:
Post a Comment