Beki Kelvin Yondani na mshambuliaji Amissi Tambwe wataikosa JKT Ruvu kesho.
Wawili hao wanaikosa mechi hiyo wakati Yanga ikipambana kupata pointi tatu muhimu za Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Yondani ni majeruhi na Tambwe ana kadi tatu za njano hivyo wote wataikosa mechi hiyo.
Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro ameiambia SALEHJEMBE kuwa wawili hao tayari wanajua hawatacheza.
"Wao wanajua na ndiyo hali halisi, lakini Yanga tuna kikosi kipana, wako watakaowasaidia na watapambana kwa ajili ya klabu.
"Lengo letu ni kushinda na kupata pointi tatu kwa kuwa tunajua ushindani ni mkali, utaona hata tofauti ya pointi ni chache sana.
"Hivyo lazima tupambane kuhakikisha tunashinda na halitakuwa jambo lahisi lakini tunakiamini kikosi chetu na tutapambana vilivyo," alisema Muro.
0 COMMENTS:
Post a Comment