Kiungo Mwinyi Kazimoto ndiye
pekee alibaki kati ya wachezaji ambao walikuwa hawajaripoti kambini katika
kikosi cha Taifa Stars.
Mwinyi anayekipiga Al Markhiya
ya Qatar alitarajia kujiunga na Stars leo mjini Mwanza.
Wachezaji wengine wanaocheza
soka la kulipwa nchini DR Congo, Mwana Samatta na Thomas Ulimwengu pia Juma Luizio
anayekipiga nchini Zambia katika kikosi cha Zesco.
Tayari Stars iko Mwanza tayari
kuivaa Malawi katika mechi ya kirafiki itakayopigwa Jumapili.
Stars inajiandaa na mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Malawi ambayo itakuja na zaidi ya wachezaji sita wanaocheza nje ya nchi hiyo.
Wengi wa wachezaji wake
wanacheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini pia Msumbiji.
0 COMMENTS:
Post a Comment