Klabu ya AC Milan imetangaza nia ya kujenga
uwanja wake mpya ambao unaaminika utakuwa wa kisasa zaidi.
Uwanja huo hautakuwa mrefu sana kwenda juu kwa
kuwa sehemu yake ya uwanja itakuwa imechimbiwa chini tofauti na viwanja
vingine.
Pia uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza watu
48,000 tu katikati ya hoteli kadhaa pamoja na majengo ambayo kutakuwa na maduka
ya huduma mbalimbali yaliyouzunguka uwanja huo.
Imeelezwa kuwa uwanja huo hautakuwa ukiruhusu kelele za mashabiki kutoka nje na kuwasumbua wakazi wengine wa jiji la Milan. Utakuwa umejengwa katika uwezo wa kuzuia sauti hizo kutoka nje.
0 COMMENTS:
Post a Comment