Mkuu
wa kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro alikuwa kama mtu aliyepagawa baada
ya Yanga kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara.
Yanga
imetwaa ubingwa huo baada ya kuitwanga Polisi Moro kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Muro
alikuwa akiwangoza mashabiki wa Yanga huku akiwasha baadhi mwanga maalum ambao
hutumiwa na mashabiki kushangilia.
Mashabiki
wengine walikuwa wakishangilia pamoja naye huku wengine wakimpiga picha.
Mara
kadhaa, Muro amekuwa akitamba kwamba Yanga ni ya kimataifa na leo alionekana
kuwa na furaha zaidi kuthibitisha kauli yake hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment