Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga ana mambo
yake, sasa anawataka Simba wavae jezi za njano na kijani, ili wapate msaada.
Yanga imemaliza kazi kwa kutwaa ubingwa wa
Tanzania Bara, hivyo Jerry Muro anaamini ni wakati mzuri wa kuisaidia Simba
kama watakubali hayo masharti.
“Simba ni watani zetu, tunaweza kuwasaidia na
hatuna matatizo hata kidogo. Kitu kikubwa wakubali kuvaa jezi za njano na
kijani.
“Sisi tutawasaidia kumfunga Azam FC ili wao
wapate nafasi ya pili.
“Haya ni masharti, wakikubali na sisi
tutawasaidia. Nafikiri hilo liko wazi kabisa,” alisema Muro.
Muro amekuwa akiwaudhi Simba kutokana na neno
lake la kusema ni “wa mchangani”.
Simba inapambana na Azam FC kuwania nafasi ya
pili ili ishiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.
Mimi YANGA damu lakini nataka AZAM awe mshindi wa pili.
ReplyDeleteAZAM kazeni buti.