Kocha
Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, ametoboa kilichoifanya timu hiyo kupoteza
mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City uliopigwa juzi Jumamosi kwenye
Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo Simba ilipigwa mabao 2-0.
Simba
msimu huu imekuwa ‘mteja’ kwa Mbeya City. Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza,
ilikumbana na kipigo cha mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na juzi
ikalambishwa dozi tena.
Matola
alisema mchezo ulikuwa mzuri, lakini walikamatwa katika sehemu ya kiungo huku
akiitaja pia ‘sub’ ya beki na nahodha wa timu hiyo, Hassani Isihaka aliyeumia,
iliharibu mipango yao yote.
“Mchezo
ulikuwa mzuri kiujumla kwa sababu ukiangalia Mbeya hawakutukamia sana, lakini
tulikuwa na tatizo kidogo katika sehemu ya kiungo, wapinzani wetu ‘walituwini’
sana eneo hilo na kufanikiwa kushinda mchezo, tunawapongeza na tunajipanga upya
kwa mchezo ujao.
“Sub
ya Isihaka pia tulifanya bila kuipanga, kwa hiyo ikatuvurugia hesabu zetu,
lakini ndivyo soka lilivyo, ‘sometimes’ tunatakiwa kukubali matokeo na
kuangalia mipango ya mbele,” alisema kocha huyo aliyechukua jiko hivi karibuni.
Matokeo
hayo yanaifanya Simba iifukuzie Azam kwa tofauti ya pointi saba katika nafasi
ya pili, ikiwa imebakiza mechi nne kabla ya kumaliza ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment