Beki kisiki na nahodha wa kikosi cha Yanga, Nador Haroub ‘Cannavaro’, ametamka kuwa
alipata wakati mgumu katika kumkabili straika wa Etoile du Sahel ya Tunisia,
Bounedjah Baghdad kutokana na mshambuliaji huyo kuwa na uwezo mkubwa wa
kupambana na mabeki.
Beki
huyo ambaye alilazimika kutolewa uwanjani baada ya kuumia enka ya mguu wake wa
kulia, ndiye alikuwa shujaa wa timu hiyo baada ya kufanikiwa kuifungia bao kwa
mkwaju wa penalti katika mchezo huo ambao uliisha kwa sare ya 1-1.
Cannavaro alisema safu yao ya ulinzi ilipata wakati mgumu wa kukabiliana na
mshambuliaji huyo kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao wa kukabiliana na
mabeki.
“Yule
jamaa Baghdad achana naye kabisa kwani ni bonge la straika kutokana na kiwango
chake kwa sababu anaweza kukaa na mipira, kupiga chenga na hata kukaa katika
nafasi nzuri. Alitupa kazi kubwa katika kumkabili, jambo ambalo lilitufanya
tutumie akili nyingi zaidi ya kumzuia.
“Lakini
tunashukuru kwa kucheza naye ambapo hakuleta madhara makubwa kwa upande wetu
ila alichangia kwa kiasi kikubwa katika majeraha yangu haya ya enka, ambayo
nimeyapata,” alisema Cannavaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment