April 27, 2015



Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema hata kidogo hawajakata tamaa kuendelea kuifukuzia nafasi ya pili.


Matola amesema wanachoamini kama watashinda mechi zote mbili walizobakiza wanaweza kuwa na nafasi.

"Hatuwezi kujua matokeo yafuatayo yataleta nini, sisi tunachotakiwa ni kuhakikisha tunashinda mechi zilizobaki.

"Katika soka si lahisi kukata tamaa halafu ukasema unahitaji kupata kitu kizuri," alisema nahodha huyo wa zamani wa Simba.

"Tulichoamua ni kupambana kwa kucheza soka safi, soka la kusaka ushindi.Baada ya hapo, mambo mengine tutajua huko mbele."

Simba iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 41 huku Azam FC ikiwa na 45 katika nafasi ya pili. Hata hivyo, Azam FC wana mchezo mmoja mkononi.

Katika mechi tatu walizobaki Azam FC, moja watakutana na Simba na inategemea, kama watapoteza hiyo na nyingine moja wanaweza kutoa nafasi kwa Simba.



iungo nyota wa Chelsea, Eden Hazard ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi kuu England kwa wachezaji wote wa kulipwa.


1 COMMENTS:

  1. Simba ni wa kusoma namba tuuuuuuuuuuuuuu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic