Kiungo
nyota wa Chelsea, Eden Hazard ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi kuu
England kwa wachezaji wote wa kulipwa.
Hazard
ameshinda tuzo hiyo ya PFA kwa mwaka 2015.
Raia
huyo wa Ubelgiji mwenye miaka 24 tayari ameisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa
Capital One na yuko njiani kuisaidia kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England.
Tayari
ameshafunga mabao 18 akiwa na Chelsea msimu huu na anazidi kuonekana ni
mchezaji tegemeo zaidi huku Chelsea ikiutaka ubingwa huo kwa udi na uvumba. Mara
ya mwisho iliubeba mwaka 2010.
0 COMMENTS:
Post a Comment