Wakati Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, akitarajiwa kufunga ndoa, kocha mkuu wa timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovic, amefunguka kuwa amefurahia kitendo hicho.
Kocha huyo anatarajiwa kufunga ndoa keshokutwa Ijumaa, hivyo hatakuwa na kikosi hicho kitakaposhuka dimbani kuivaa Kagera Sugar, Kambarage, Shinyanga.
Kopunovic alisema anafurahia maamuzi ya mwalimu mwenzake na anamtakia kila la kheri katika maisha mapya ya ndoa ambayo anatarajiwa kuyaanza.
“Kiukweli nafurahia uamuzi wa rafiki na mwalimu mwenzangu Suleiman Matola, kwa kuchukua uamuzi wa kufunga ndoa ni hatua moja na nzuri katika maisha ambayo binadamu tunapitia.
“Namtakia kila la kheri katika maisha mapya ya ndoa ambayo anatarajiwa kuyaanza hivi karibuni na hata mchezo wetu ujao dhidi ya Kagera hatutakuwa naye, cha msingi ni kumuombea heri afanikiwe kufanikisha shughuli yake kwa amani na upendo,” alisema Kopunovic.








0 COMMENTS:
Post a Comment