April 20, 2015


Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), leo hii limepokea maombi toka Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), likiitaka Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ngazi ya vilabu yatakayotimua vumbi kuanzia mwezi Julai mwaka huu.


Kufuatia maombi hayo ya uenyeji wa michuano ya CECAFA kwa ngazi za vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame CUP), TFF inatafakari juu ya maombi hayo na itayatolea maamuzi.


Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye ameishathibitisha kuwa michuano hiyo itafanyika Tanzania Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic