April 2, 2015

Mashabiki na wanachama wa Yanga katika mji wa Tunduma wameonyesha mapenzi ya dhati kwa wenzao waliokuwa njiani kwenda Zimbabwe kuiunga mkono Yanga ikipambana na FC Platinum.



Walijitokeza na kuwapa maji, pia kuzungumza nao na kuwapa moyo kwamba wanawaunga mkono kwenda kuipa nguvu Yanga ikipambana katika mechi hiyo muhimu ya Kombe la Shirikisho. Mechi ya kwanza, Yanga ilishinda kwa mabao 5-1.

Msafara huo wa makamanda hao wa Yanga ulipita Tunduma jana na leo tayari umekanyaga ardhi ya Zimbabwe na unaendelea na safari.

Taarifa zimeeleza msafara huo unatarajia kuwasili mjini Bulawayo saa 12 jioni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic