May 15, 2015


Adidas imempa nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard viatu maalum ambavyo atavitumia wakati wa kuwaaga mashabiki wa timu hiyo.


Viatu hivyo atavivaa katika mechi zake mbili zilizobaki za Liverpool akianza na ile ya Jumamosi dhidi ya Crystal Palace ambayo ni muhimu sana kwa kuwa ndiyo ya mwisho kwake katika Uwanja wa Anfield.


Baada ya mechi hiyo, Gerrard atavivaa tena viatu vya aina hiyo katika mechi yake ya mwisho kabisa akiwa na Liverpool ambayo watacheza dhidi ya Stoke City wakiwa ugenini.

Gerrard anaondoka Liverpool na kwenda kujiunga na LA Galaxy ya Marekani.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic