Uongozi wa Simba umekaa chini kujadili kuhusiana na Kocha Goran Kopunovic ambaye anaonekana anawaletea 'mapozi'.
Kopunovic ametaka kupewa dola 50,000 (zaidi ya Sh milioni 100) ili asaini mkataba mpya Simba, jambo ambalo uongozi wa klabu hiyo umeona si sahihi.
Uongozi wa Simba pamoja na viongozi wengine wa kamati ya utendaji wamekutaka jioni hii kwa ajili ya kujua mustakabari wa kocha huyo.
"Kuna mkutano wa viongozi wamekutana usiku huu, lengo ni kujua wafanye nini. Inawezekana wakaamua kutafuta kocha mwingine.
"Inaonekana kama Kopunovic anawasumbua na wao wanaona hakuna haja ya kuendelea kusumbuka naye," kilieleza chanzo.
Kocha huyo raia wa Serbia ameiwezesha Simba kushika nafasi ya tatu, baada ya hapo ametaka aongezewe mkataba mpya lakini lazima alipwe kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kimeonekana ni kikubwa kwa Simba.
Tayari kocha huyo nchini Hungary ambako ndipo yalipo makazi yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment