KIGGI |
Wachezaji wa zamani wa
Yanga, Abubakar Mtiro na Kiggi Makassy, wamemaliza mikataba katika klabu zao za
Kagera Sugar na Ndanda FC lakini bado wana hamu ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu
ujao.
Msimu uliopita, Mtiro
alimudu kucheza vizuri beki ya kushoto katika kikosi cha Kagera kiasi cha
kuitwa Taifa Stars, lakini Kiggi pia aliisaidia Ndanda kubaki ligi kuu baada ya
kujiunga nayo Desemba, mwaka jana.
Kidogo Mtiro anaonekana
umri umemtupa kwani ana miaka 32, tofauti na Kiggi mwenye miaka 23, wote
wamesema wapo huru na wangependa kujiunga na klabu yoyote itakayowataka.
“Mkataba wangu tayari
umeisha, najiona bado nina nguvu za kuendelea kucheza, hivyo kama kuna timu
inanihitaji nipo tayari kujiunga nayo lakini hata Kagera naweza kuendelea nayo
pia,” alisema Mtiro.
Kwa upande wake, Kiggi
aliyewahi pia kuitumikia Simba, alisema: “Mimi nimeshamalizana na Ndanda na
hapa sasa natazama ustaarabu mwingine kwa timu nyingine ya ligi kuu, ila naweza
pia kubaki Ndanda.”
0 COMMENTS:
Post a Comment